Image
Image

KCMC inakabiliwa na tatizo la vitanda vya kufanyia upasuaji.

Hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro inakabiliwa na tatizo la vitanda vya kufanyia upasuaji hali ambayo inazidi kuchangia ongezeko la msongamano wa wagonjwa wodini huku baadhi ya wagonjwa wakilazimika kulala kwenye varanda kusubiri huduma.
Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya KCMC Prof Giliad Masenga ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa Blanketi maalumu za wagonjwa kutoka benki ya Diomond Trust na kuwa vitanda vinavyotumika kwa sasa ni chakavu.
Amesema idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji ni kubwa na kwamba vitanda vilivyopo ni vya zamani na kwamba ununuzi wa vitanda hivyo ni gharama kubwa ambapo kitanda kimoja kinagharaimu zaidi ya shilingi milioni 40.
Mapema akikabidhi shuka hizo maalumu za wagonjwa 100 zenye thamani ya shilingi milioni 5 kati ya shuka 2000 zinazohitajika hosptalini hapo meneja wa benk ya Diomond Trust tawi la Moshi Bw.John Robert amesema msaada huo ni sehemu ya faida waliyopata na kutokana na kazi wanayoifanya.
Akizungumzia hali ya msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo afisa uhusiano wa hospitali ya rufaa ya KCMC Bw.Gabriel Chiseo amesema tayari wako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa idara ya wagonjwa wa dharura ambayo inatarajia kuanza kutumika mwezi January mwakani 2016.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment