Wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura ya kumchagua mbunge
wa jimbo la Masasi licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza ikiwamo ya
mawakala wa CUF kukataliwa kwa sababu za kutokidhi vigezo katika mchakato huo.
Baadhi ya wananchi waliofika katika kituo cha kupigia
kura cha Msufini one wamesema kitendo hicho kimelenga kuvuruga uchaguzi huo.
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi jimbo la Masasi mjini
Shaibu Dadi amesema wasimamizi wamelazimika kumkataa na kwamba hatambuliki
kisheria kwasabu hana kiapo cha kuwa wakala.
Katika hali isiyo ya kawaida wafuasi wa chama cha wananchi
CUF walivamia nyumbani kwa katibu wa UWT kata ya Mkomaindo na kudai kuna
masanduku ya kura yamefichwa hali iliyolazimu jeshi la polisi kuzingira nyumba
kwa usalama.
Jeshi la polisi limeonekana likivinjari huku na kule
kulinda usalama, vyama vinavyogombea nafasi ya umbunge ni CCM, CUF, Chadema,
ACT na NLD.
0 comments:
Post a Comment