Image
Image

Latest News:Mapigano ya wakulima na wafugaji waziri Nchemba achukua hatua Mvomero.



Mgogoro wa wakulima na Wafugaji:Hii leo nimefika Mvomero kijiji cha DIhinda kata ya Kanga kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya tukio baya la mauaji,Kujeruhi BInadamu na Wanyama lililotokea Desemba 12/2015.
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima,Hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua,Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi.Tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria."
Nimeagiza kupitia kwa Mkuu wa wilaya na kamati yake ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Mvomero(kwa husika maeno yote ya Nchi yetu) kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro,pili wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.
Kwa walio jeruhiwa,nimeagiza wapatiwe matibabu kwanza bila kuchelewa na hatua za kisheria kwa wenye hatia zifuate.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment