Image
Image

Meneja Mkuu na Mhasibu mbaroni kwa ubadhilifu wa Shilingi Milioni 98 na Laki- 2 Kilimanjaro.



Meneja Mkuu na Mhasibu Mkuu wa Mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Hai Wilaya  y a Hai Mkoani Kilimanjaro wamekamatwa na polisi kwa maagizo ya Halmashauri ya wilaya hiyo,kwa tuhuma za ubadhilifu wa  Shilingi Milioni  98  na Laki- 2  ambazo waliagiza  Mita   za maji  kutoka Ujerumani ambazo hazijulikani zilipo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa halmashauri hiyo ambayo mamlaka hiyo iko chini yake,SAIDI MDERU amesema, Meneja Mkuu huyo ROGERS MARANDU na Mhasibu Mkuu wake DEVOTA MWAMBURI waliagiza mita hizo mwaka jana  wakati wakijua  zinapatikana hapa nchini kwa ubora zaidi.
MDERU pia amesema, mamlaka hiyo inatuhumiwa kwa upotevu wa  Shilingi BILIONI  3  ambazo mwaka jana zilitengwa kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa maji katika wilaya hiyo ili huduma za maji ziwafikie wananchi walio wengi..
Mkuu wa wilaya hiyo,ANTONY MTAKA amesema, hili ni tukio la tatu la ubadhilifu katika kipindi cha mwezi mmoja Wilayani Hai na kwamba serikali itaendelea kufuatilia matumizi ya fedha na kutumbua majipu katika ngazi zote za serikali na kuwawajibisha watuhumiwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment