Image
Image

Lishe duni na mila potofu chanzo cha vifo vya wajawazito na watoto Mkoani Arusha.



Wilaya ya Longido inaongoza kwa vifo vya wajawazito na watoto Mkoani  Arusha  hali inayo tajwa kusababishwa na lishe duni,mila potofu na mazingira machafu  kwa  wanawake wa naoishi  vijijini .
Mkuu wa Wilaya ya Longido,ERNEST KAHINDI amesema familia zinazo ishi vijijini zimekuwa na tatizo la upatikanaji wa lishe bora,hasa kwa wanawake na watoto wengi  hupata mlo mmoja kwa siku  na  siyo chakula bora .
Hiyo inatokana na umasikini hivyo  Mkuu huyo wa Wilaya  amewataka wakazi wake kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na ufugaji wa kisasa ili kuongeza kipato chao .
Baadhi ya wadau wa mazingira wamesema biashara ya kuuza mkaa kwa wanawake wa Longido pia imekuwa sababu ya kuhatarisha afya zao hivyo wadau wamekuja na mbinu mbadala ya kumkomboa mwanamke kwa kuwapatia mitaji ya ufugaji wa kuku ili kuokoa afya zao kulinda mazingira na kuwakwamua kiuchumi  wanawake hao kutoka jamii za wa fugaji .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment