Taharuki imetanda baada ya meli ya royal iliyokuwa ikitokea
Unguja kuelekea Pemba kuelezwa kuwa inawaka moto huku watu wakijitahidi
kujinasua ili kunusuru maisha yao.
Wakati abiria hao wakijaribu kujinasua ndani ya meli hiyo
hatimaye Meli ya Serengeti iliyokuwa inatokea Pemba kwenda unguja imeikuta
njiani na kuanza kutoa msaada hivyo shughuli za uzimaji moto na uokozi Wa
abiria na Mali zao inafanyika hivi sasa.
Bado hakuna taarifa za watu kupoteza Maisha na Chanzo cha
Moto hakijafahamika bado licha ya kuelezwa kuwa kulianza kusikia harufu kali
ndani ya meli hiyo,ingawa tangu iondoke na abiria haikubainika kuwa ilikuwa na
hitilafu yeyote ile.
Tutawajuza baada ya Taarifa zingine tuzipatazo.
hongera kwa kaz nzur pia nawapa pole wote waliofikwa na janga hlo
ReplyDelete