Maamuzi hayo ya
mahakama kuu ya tanzania yamekuja kufuati ombi la dhama
lililowakilishwa mahakamani hapo na washitakiwa watatu wakiongozwa aliyekuwa
kamishina wa forodha wa tra Bw.Tiagi Masamaki,
Ambapo kwa mujibu wa jaji
wa mahakama hiyo bi wilfrida koroso
amesema dhamana kwa washitakiwa hao
watatu iko wazi kama watatimiza
masharti sita yakiwemo ya kulipa hundi
ya sh bilioni 2.6 kila mmoja huku pia
wakitakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiri
huku pia wakitakiwa kuwa na wadhamini watakao kuwa na uwezo wa kusain
hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.
Katika hatua nyingine
mbunge wa jimbo la ubungo mh saed kubenea amepandishwa kizimbani katika
mahakama ya hakimu mkazi kisutu dar es salaam
akikabiliwa na shitaka la kutumia lugha ya matusi kinyume na sheria .
Akisoma shitaka mbele
ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo
thomas simba, mwendesha mashitaka
wa seriakli timon vitalis ameiambia
mahakama kuwa mnamo dec 14 mwaka huu katika eneo la epz mtuhumiwa huyo alitumia
lugha ya matusi " we kibaka, we mjinga, mpumbavu , cheo chenyewe umepewa" maneno yaliyokuwa yakimlenga mkuu wa wilaya
ya kinondoni,
Ambapo kwa mujibu wa
mwendesha mashitaka huyo amesema maneno hayo yangeweza kuhatarisha amani ikiwa
ni kwa mujibu wa kifungu namba 89 (i)
a cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya
mwaka 2002 ambapo hata hivyo mshitaka huyo alikana shitaka hilo.
Mtuhumiwa huyo
alikuwa akitetewa na jopo la mawakili watano wakiongozwa na wakili peter
kibatala ambapo hata hivyo baada ya kukithi vigezo vya dhamana aliachiwa nje
kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment