Akizungumzia suala hilo wakati wa kikao cha baraza la
wafanyakazi wa wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto
katibu mkuu wa wizara hiyo dk donad mbando amesema tayari kipuri
kilichoharibika kwenye mri kimeshaagizwa nchini uholanzi.
Katika mazungumzo yake na wafanyakazi wa wizara hiyo Dk.Mbando
amewataka kupiga vita rushwa kwa nguvu zote na kuwa wawazi hasa suala la
gharama za utoaji huduma zikiwemo za kuchangia na kukiri kuwepo kwa kasoro za
kiutendaji ambazo zinafanyiwa kazi.
Baada ya mashine hizo kufanyiwa matengenezo na kutengemaa
kabla ya kuharibika tena mashine ya mri ilikuwa imetoa huduma kwa wagonjwa 270
na CT-SCAN wagonjwa 574 huku wengine wakiwa wanasubiri zamu zao.
0 comments:
Post a Comment