Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wake,
Mhe. Dkt. Suzan Kolimba waliwasili Wizarani kuanza kazi rasmi siku ya
Jumamosi tarehe 12 Desemba 2015.
Viongozi
hao wapya wa Wizara walipokelewa na watumishi kwa shangwe walipowasili
wizarani, muda mfupi baada ya kula kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Dar
es Salaam.
Siku
ya kwanza Wizarani, Waheshimiwa Mawaziri walipata fursa ya kukutana na
uongozi wa Wizara ukiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula na
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.
Joyce Mapunjo. Makatibu Wakuu hao pamoja na mambo mengine, walikabidhi
kwa Waheshimiwa Mawaziri nyaraka muhimu za Wizara zitakazowaongoza
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha,
walitumia fursa hiyo kueleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara na
masuala ambayo yanahitaji miongozo yao ili yaweze kufanyiwa kazi na
kukamilishwa.
Balozi
Mahiga na Dkt. Kolimba walipata fursa pia ya kutembelea watumishi wa
iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki siku ya tarehe 14
Desemba 2015 kwenye Jengo la Waterfront. Watumishi hao kama walivyofanya
wenzao waliwapokea viongozi wapya kwa shangwe na baadaye kufanya kikao
na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Katika
vikao vyote, Mhe. Waziri aliomba ushirikiano kutoka kwa Wakuu wa
Idara/Vitengo na watumishi wote kwa jumla ili kwa pamoja waweze kuendana
na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye kaulimbiu ya
“Hapa kazi tu”
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula aliyesimama akitoa neno kabla ya
kumkaribisha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati)
kuongea na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara hiyo. Kushoto ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza
kushoto), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi, Bw. Wilfred Masanja (wa
kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. John Ngowo
wakisikiliza kwa makini neno la ukaribisho kutoka kwaBalozi Mulamula
akimkaribisha Mhe. Waziri kuzungumza na Wakuu wa Idara/Vitengo.
Sehemu
nyingine ya Wakurugenzi walioudhuria kikao hicho, wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw.
Negel Msangi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Anisa Mbega
(katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi
Innocent Shiyo.
Home
News
Balozi Dkt. Mahiga akutana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment