Image
Image

Breaking News:Meli ya Royal iliyokuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba inaungua moto




Taharuki imetanda baada ya meli ya royal iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba kuelezwa kuwa inawaka moto huku watu wakijitahidi kujinasua ili kunusuru maisha yao.

Wakati abiria hao wakijaribu kujinasua ndani ya meli hiyo hatimaye Meli ya Serengeti iliyokuwa inatokea Pemba kwenda unguja imeikuta njiani na kuanza kutoa msaada hivyo shughuli za uzimaji moto na uokozi Wa abiria na Mali zao inafanyika hivi sasa. 

Bado hakuna taarifa za watu kupoteza Maisha na Chanzo cha Moto hakijafahamika bado licha ya kuelezwa kuwa kulianza kusikia harufu kali ndani ya meli hiyo,ingawa tangu iondoke na abiria haikubainika kuwa ilikuwa na hitilafu yeyote ile.

Tutawajuza baada ya Taarifa zingine tuzipatazo.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments:

  1. hongera kwa kaz nzur pia nawapa pole wote waliofikwa na janga hlo

    ReplyDelete