Katibu mkuu ofisi ya rais tawala za mikoa na
serikali za mitaa (TAMISEMI) Bwana Jumanne Sagini amemsimamisha kazi mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Mhandisi Mussa Natty ambaye (Pichani)
kabla ya kuhamishiwa wilayani Babati alikua mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Bwana Sagini amefafanua kuwa pamoja na kusimamishwa
kazi, Mhandisi Natty anapaswa kurudi katika halmashauri ya manispaa ya
Kinondoni na kusubiri uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.
Ametaja tuhuma hizo kuwa ni pamoja na usimamizi
mbaya uliosababisha barabara za manispaa ya Kinondoni kujengwa chini ya kiwango
na kutowachukulia hatua watendaji wa manispaa waliokua chini yake, ukosefu wa
uadilifu katika ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa bahari la Coco Beach na
malalamiko ya wananchi juu ya viwanja katika eneo la Kinondoni ulioambatana na
usimamizi duni wa watumishi hasa wa sekta ya mipango miji na ardhi.
0 comments:
Post a Comment