ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Philemon Mollel ‘Monaban’, ameibuka na madai mazito kwa Jeshi
la Polisi kuwa walichangia kushindwa kwake na Godbless Lema wa Chadema.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jijini hapa juzi, wapigakura
105,800 walijitokeza kati ya 317,814 waliojiandikisha ambapo kura halali
zilikuwa 104,353 huku 1,447 zikiharibika.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha, Juma Iddi, alimtangaza Lema kuwa mshindi wa kiti cha ubunge kwa kupata
kura 68,848 sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mollel 35,607 sawa na asilimia
34, Navoi Mollel (ACT-Wazalendo) 342, Zuberi Hamisi (CUF) 96 na Makame Jaria
(NRA) 41.
Uchaguzi huo ulifanyika baada ya kuahirishwa awali kutokana
na kifo cha aliyekuwa mgombea wa ACT-Wazalendo, Estomih Mallah aliyefariki
kabla ya Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumzia matokeo hayo, Mollel alisema hakuridhishwa na
namna ulivyoendeshwa na kusimamiwa na vyombo vinavyohusika.
Mollel ambaye pia ni Kamanda wa Vijana wa CCM Mkoa wa
Arusha, alidai kuwapo kwa kasoro nyingi wakati wa kampeni na upigaji kura.
“Kulikuwa na gari Noah ya diwani wa Chadema ilipita baadhi
ya vituo vya kupigia kura na kudai inawapelekea chakula mawakala. Lakini gari
hiyo tumeambiwa ilikuwa na kura bandia zilizofanikiwa kuingizwa kwenye
masanduku,” alisema Mollel.
Pia alilitupia lawama Jeshi la Polisi mkoani hapa, kwamba
walizunguka na magari yenye maji ya kuwasha, huku mengine yakiwa na polisi
mitaani jambo ambalo lilichangia wapigakura kujitokeza wachache, hususan
wanawake na wazee.
“Wazee na akina mama waliogopa kwenda kupiga kura kutokana
na magari ya polisi na askari wengi walioonekana mitaani. Hapakuwa na vurugu
zozote, kwanini kuwatisha wananchi kwa silaha na vifaa vingine vya kivita?”
alihoji Mollel.
MBOWE ANENA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye alikuwa Chuo
cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Njiro jijini wakati matakeo hayo
yakitangazwa, alisema wakazi wa Arusha wameweza kuzungumza na kupaza sauti zao
kupitia sanduku la kura.
“Ushindi wa Lema na kutangazwa kuwa mbunge mteule,
umeonyesha kwa mara nyingine umuhimu wa kuheshimu sanduku la kura kama msingi
wa amani na utulivu katika Jiji la Arusha,” alisema Mbowe.
Kwa upande wake, Lema aliwashukuru wananchi wa jimbo hilo
kwa kupiga kura bila ubaguzi wa kabila
0 comments:
Post a Comment