Image
Image

Polisi wa Burundi watia mikononi silaha kadhaa za kivita katika mtaa mmoja wa Bujumbura.


Kikosi cha polisi nchini Burundi kimeripoti kukamata silaha kadhaa za kivita zilizokuwa zimefichwa katika mtaa mmoja wa mji mkuu wa Bujumbura.
Kikosi hicho cha polisi kilifanikiwa kuzitia mikononi silaha hizo hapo jana wakati wa operesheni iliyofanyika katika mtaa wa Ngagara.
Wakaazi wa mtaa huo walitoa taarifa kwa polisi kuhusiana na maficho ya silaha hizo na kuwawezesha kuzikama kwa urahisi.
Silaha hizo zilizokamatwa zilikuwa ni bunduki 5 aina ya Kalashnikov, kombora 1, mabomu 29 pamoja na risasi nyingi.
Wakati huo huo, washukiwa wawili pia walitiwa mbaroni baada ya kuhusishwa na umiliki wa silaha hizo.
Ngagara ni mojawapo ya mitaa iliyofanya maandamano ya kupinga uongozi wa rais Nkurunziza kwa muhula wa tatu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment