Image
Image

Kesi inayo wakabili wafanyakazi wa TRA kusikilizwa Januari 13 Mwakani.



Na Nyakongo Manyama-Maelezo.
Kesi inayowakabili wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kusikilizwa tena January 13, 2016
Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es salaam Wakili wa Serikali Bi. Dianna  Lukondo amesema kuwa  kwa leo Kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa dhamana kwa washtakiwa na hivyo imeshindikana kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika.
“Upelelezi haujakamilika hivyo kesi itasikilizwa tena Januari mwakani ” alisema Dianna.
Kesi hiyo inawakabili aliyekuwa  Naibu Kamishna TRA  Tiagi Masamaki, meneja wa kitengo Huduma kwa Wateja  Habibu Mponezya, na wengine ni  Khamis Omary, Eliaichi Mrema, Burton Kaisi, Harun Mpande na Raymond Louis.
Washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi, wakidaiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam yaliosababisha  ukwepaji wa ushuru zaidi ya sh. Bilioni 80
.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment