Image
Image

Rais.Magufuli afanya mazungumzo na Spika wa Seneti na mjumbe Maalum wa rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa seneti ya Burundi  na mjumbe maalum wa rais wa Jamhuri ya Burundi Reverien Ndikuriyo Ikulu Jijini Dar es Salaam juu ya hali ilivyo nchini Burundi na jitihada zinazochukuliwa na tanzania ambayo ni mwenyekiti wa jumuia ya Afrika mashariki ili kusaidia uwepo wa hali ya utulivu nchini humo.

Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nje Afrika Mashariki kikanda na kimataifa balozi Augustine Mahiga kilicholenga kuzungumzia hali ya kisiasa nchini Burundi,serikali ya Burundi imeihakikishia tanzania kuwa iko tayari kufanya mazungumzo ya amani na wadau wote wa siasa nchini Burundi.

Balozi mahiga ameongeza kuwa katika kikao hicho ujumbe huo umeelezea hatua ya bunge la nchi ya Burundi kupinga uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa afrika wa kutaka kupeleka majeshi yake nchini Burundi kwa kuwa inaamini kuwa hakuna hali ama dalili za kutokea kwa mauaji ya kimbari kama ya rwanda na kwamba kuna utulivu nchini humo tofauti na wasiwasi wa umoja wa Afrika,jumuiya za kimataifa hasa umoja wa ulaya,na kwa kiwango fulani umoja wa mataifa unaotoa msukumo wa kutaka kuyapeleka majeshi ya kulinda amani nchini burundi.

Kuhusiana na suala la bunge la Burundi kupinga kupelekwa kwa majeshi ya umoja wa afrika nchini humo balozi Augustine Mahige amesema Rais Dr.John Pombe Magufuli ametoa mapendekezo.

sambamba na mapendekezo hayo rais magufuli amemuagiza balozi maiga kwenda nchini burundi kutazama, kujiridhisha na kutathmini hali halisi ilivyo hususani katika suala la amani hasa ulinzi na usalama wa raia si katika jiji la Bujumbura pekee bali pia maeneo mengine ya nchi hiyo ili kufahamu sababu zinazowafanya warundi kukimbia nchi yao na kukimbilia tanzania kama wakimbizi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 22,2015.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 22,2015.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment