Image
Image

Wazazi waiomba serikali kuongeza idadi ya walimu katika shule Wilayani Muheza.



Baadhi ya wazazi wa vijiji mbali mbali  katika Kata ya Kwempapayu Wilayani Muheza wameiomba Serikali kuongeza idadi ya walimu katika shule hiyo kufuatia baadhi yao kulazimika kuhamisha watoto wao na kuwapeleka katika shule nyingine zilizopo jirani na Kata hiyo hatua ambayo imesababisha mahudhurio shuleni kuwa kati ya wanafunzi 20 hadi 30 kwa siku.
Wakizungumza katika Kijiji cha Kwempapayu kuhusu tatizo hilo,Afisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Kwempapayu,MWANAID MWAIMU pamoja na baadhi ya wazazi wamesema ,   hatua hiyo imesababisha wananfunzi kuathirika kitaaluma kwa sababu ya kuosa masomo wanapokuwa darasani .
Akithibitisha  tatizo hilo,Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kwempapayu,ALLY CHOGOGWE amesema  walimu  waliopo ni wanne na Darasa la Kwanza hadi la pili anafundisha mwalimu mmoja na  Darasa   la tatu hadi la Saba walimu wanaofundisha ni watatu .
Kufuatia hatua hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,ADRIAN JUNGU amekiri kuwepo kwa uhaba mkubwa wa walimu wilayani humo na amesema wamejiwekea mikakati ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne na Sita kutoka katika vijiji vilivyoathirika na tatizo hilo ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment