Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iko tayri kushirkiana
na wawekazaji wa nje kuhuus suala la uchimbaji wa mafuta na gesi kwa vile
ndio tegemeo kubwa la uchumi wa nchi.
Dr.Shein ametoa changamoto hiyo Ikulu Zanzibar
alipokutana na wataalamu kutoka china wa kampuni ya china OFFSHORE OIL
ambao walifika Ikulu kuonana naye na kufanya mazungumzo kuhusu
uendelezaji wa ushirikiano wa nchi mbili hizo.
Amemsmea china na Zanzibar zina ushirkiano wa miaka
mingi katika nyanyja mbalimbali hivyo ujio wa kampuni hiyo ni miongoni mwa
hatua hizo za ushirkiano,hata hivyo Dk.Shein akasisitiza kuwa china pia
inaangalia uwezekano wa kusaidia wazalendo wa Zanzibar kufaidika na
elimu ya taaluma ya uchimbanji wa mafuta na gesi.
Serikali ya Zanzibar imekusudia kuimarisha
sekta hiyo na tayari imekubaliana na serikali ya muungnao ili suala hilo
liwemikononi mwa Zanzibar,
Kwa upande wake makamu wa rais wa kampuni hiyo
ya CNNOG Bw. CUI HANYON amesema kampuni yao itataoa ushirkiano kwa
SMZ katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu na ushauri elekezi
na kuahidi kuwa pamoja na Zanzibar katika kufufua uchumi wake.
Ujumbe huo wa china ulifutana na balozi mdogo wa
china anayefanya kazi zake Zanzibar na kampuni hiyo tayari inaendesha
miradi yake nchi mbalimbali ikiwamo ASIA,ULAYA na AFRIKA ikiwemo
GABON,NOGERIA,KENYA na UGANDA.
0 comments:
Post a Comment