Mazungumzo ya amani ya Yemen yanayosimamiwa na Umoja
wa Mataifa nchini Uswisi yanazorota kutokana na mvutano kuhusu kuachiwa huru
mafisa wa ngazi ya juu wa serikali wanaoshikiliwa na wanamgambo wa
Houthi.
Mazungumzo ya amani ya Yemen yanayosimamiwa na Umoja
wa Mataifa nchini Uswisi yanazorota kutokana na mvutano kuhusu kuachiwa huru
mafisa wa ngazi ya juu wa serikali wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Houthi.
Mazungumzo kati ya wawakilishi wa serikali na wa
wanamgambo wa shiya-Houthi wanaodhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Yemen,ikiwa ni
pamoja na mji mkuu Sanaa yameanza tangu jumanne iliyopita katika mji uliowekwa
siri wa Uswisi.
Masaa machache kabla ya mazungumzo hayo kuanza,
makubaliano ya kuweka chini silaha yakaanza kufanya kazi nchini humo,lakini
kambi mbili zinazohasimiana zimeshaanza kulaumiana kuyaendeya kinyume
makubaliano hayo.
Lengo la mazungumzo ya Uswisi ni kusaka namna ya
kumaliza mzozo ulioangamiza maisha ya karibu watu 6000 na mamilioni kuyapa
kisogo maskani yao tangu Saud Arabia ilipoamua kuingilia kati mwishoni mwa
mwezi wa march mwaka huu.
Duru za karibu na mazungumzo zinasema majadiliano ya
ana kwa ana kati ya pande hizo mbili yamesitishwa tangu jana usiku.
Juhudi za Upatanishi zimeshika kasi.
Wahouthi wamekataa kuwaachia huru,kama wanavyodai
wawakilishi wa serikali ya rais Hadi,maafisa kadhaa wa ngazi ya juu ikiwa ni
pamoja na waziri wa ulinzi Mahmoud al Subaihi na nduguye rais
Hadi,Nasser.Maafisa hao wawili waliokuwa wakiongoza shughuli za upelelezi
katika majimbo ya Aden,Lahej na Abyan wanashikiliwa na wanamgambo wa Houthi
tangu mwezi Marchi uliopita.Wahouthi wanasema watakuwa tayari kuwaachia huru
mara baada ya makubaliano ya kudumu ya kuweka chini silaha,yatakapojadiliwa.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini
Yemen,Ismael Ould Cheikh Ahmed wa Mauritania yuko mbioni tangu wakati huo
kujaribu kusawazisha mvutano huo.
Zoezi la kuwaachia huru wafungwa linaendelea
Nchini Yemen kwenyewe mapigano yameripuka usiku wa
jana kuamkia leo katika eneo la Marib,umbali wa kilomita mia moja toka mji mkuu
Sanaa.Watu wasiopungua 15 wameuwawa kutoka pande zote mbili.
Ndege za kivita zinazoongozwa na Saud Arabia nazo
pia zilishiriki katika mashambulio katika mkoa wa Hajja karibu na mpaka wa Saud
Arabia.
Katika hali kama hii,zoezi la kubadlishana wafungwa
lililofanyika alfajiri kati ya wanamgambo wa Houthi na vikosi vya
Kusini,vinavyoshirikiana na serikali ya Hadi,ni tukio pekee la kutia moyo
machoni mwa wapatanishi wa kimataifa.
Mashahidi wanasema wahouthi wamewaachia huru wakaazi
265 wa kusini mwa Yemen na badala yake vikosi vya Kusini vikawaachia huru
wafuasi 300 wa Houthi.
0 comments:
Post a Comment