Wale watakaohudhuria wanatarajia kujadiliana
pendekezo la kutaka kuwapa watu kutoka Syria walio katika kambi nchini Uturuki
makaazi moja kwa moja.
Hata hivyo Chansela wa Ujerumani Angela Merkel,
aliyetoa pendekezo hilo, anakabiliana na upinzani mkali kutoka mataifa mengine
ya Ulaya.
Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya unaopaswa
kufanywa Alhamisi unatarajiwa kumulika tatizo la uhamiaji ambalo limegawa
wanachama wa Jumuiya hiyo.
Watu wengi wamewasili Ulaya mwaka huu, jambo ambalo
limeyafanya mataifa mengine kujenga nyua kwenye mipaka yao ili kuanza kuthibiti
mienendo ya wahamiaji hao.
Wakati huohuo mataifa mengine wanachama yameanza
kupuuza mapatano ya Schengen, ambayo yanaruhusu raia wa mataifa hayo ya ulaya
kutembeleana bila vibali au mtu kupata visa moja ya kutembelea mataifa yote
wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Pendekezo hilo mpya litashuhudia mataifa wanachama
wa Jumuiya ya Ulaya yakiwakubali wakimbizi wa Syria wanaotoka kambi za Uturuki
moja kwa moja chini ya mpango wa kujitolea.
Inatarajiwa kuwa mpango huo utasitisha watu kusafiri
mwendo hatari kupitia bahari hadi Ugiriki na pia wanachama wa Jumuiya hiyo kufurahia
mpango huo kuliko kupokea idadi ya watu ambayo wamelazimishiwa.
Mwezi uliopita Uturuki na viongozi wa Ulaya
walikubaliana kuwa Uturuki itawazuia wahamiaji kuondoka nchini mwao ambapo
mataifa ya Ulaya nayo yatalegeza masharti ya kifedha na kisiasa kwa Uturuki.
Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya utajadiliana
jinsi ya kuunda kikosi cha muungano huo cha kushika doria fuo za mataifa hao na
njia za kuthibiti mipaka yake.
Vita dhidi ya ugaidi ni swala ambalo litamulikiwa
pia katika mkutano huo kwa kuwa imethibitishwa sasa kuwa wawili kati ya
washambulizi waliohusika katika shambulio la Paris Ufaranza walitumia njia
inayofuatwa na wahamiaji kufika Ufaransa.
Wahamiaji wengi wanatoroka manyumbani kwao kutokana
na ghasia katika mataifa kama vile Syria, Iraq na Afghanistan, wakitafa kufika
Ulaya.
0 comments:
Post a Comment