Zoezi la bomoabomoa linaloratibiwa na Manispaa ya Kinondoni limeingia katika hatua ya Pili ambapo limewakumba wakazi waishio katika Bonde la Mkwajuni na wakazi waishio maeneo hayo kubomolewa nyumba zao.
Mwanzoni
mwa zoezi hili la bomoabomoa Kamishna Ardhi nchini Dk
Moses Kusiluka aliweza kulitolea amefafanua na kusema kuwa zoezi la
uboaji huo halijaanza leo wala jana ila ni muendelezo na kusema kuwa zoezi hilo
wanalifanya kwa waliokiuka taratibu na sheria kwa kujenga maeneo ya
wazi,wavamizi wa maeneo na kujenga bila kibali na waliokwisha wekewa
alama ya X wataondolewa katika maeneo hayo.
Alisema
katika zoezi la uvunjaji wanafuata sheria na taratibu kwani zoezi hilo hali
mgusi masikini wala tajiri ila kama umekiuka taratibu na sheria ndio ina fuata
mkondo wake.
Alieleza
kwa kina kuwa zoezi hilo ni Endelevu
ambapo linahusisha wilaya tatu za Temeke,Ilala,Kinondoni hivyo akatoa wito kwa
waliokwisha tahadharishwa kuondoka maeneo ambayo sio rasmi wafanye hivyo mara
moja kabla hawajafikiwa na zoezi hilo la ubomoji.
Leo
katika zoezi la bomoabomoa walidai kutokupatiwa taarifa yeyote na uongozi wa
serikali ya mtaa kuwa kuna zoezi hilo linakuja kuanza waondoke maramoja.
Watoto
wadogo wamekuwa nao niwahanga katika zoezi hilo ambapo wameonekana wakilia kwa
kinachoendelea huku wazazi wao wakipaza sauti kwa serikali licha ya kupewa onyo
na serikali la kujiwajibisha kabla ya kuwajibishwa.
Je
Tahadhari ya serikali na Mamlaka husika inayo tolewa juu ya kuondoka maeneo
yasio rasmi yanapuuzwa ama wananchi hawajajua nini maana ya kukaa maeneo
hayo???.
0 comments:
Post a Comment