Serikali imesema walimu wakuu wote nchini katika shule
za msingi wataondolewa kwenye nafasi hiyo endapo wanafunzi watakaofika darasa
la tatu hawajui kusoma wala kuandika .
Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Elimu STELLAH
MANYANYA wakati wa makabidhiano ya madawati Elfu-Moja kwa shule za msingi
kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Naibu Waziri wa Elimu amesema Serikali kamwe haitavumilia
hali hiyo .
Madawati hayo yametolewa na wawekezaji mbalimbali
katika kusaidia sekta ya Elimu na kukabidhiwa kwa Mamalka ya Elimu Tanzania TEA
kwa ajili y a baadhi ya shule za msingi za Dar es Salaam na Pwani.
Nchi nzima ina tatizo la upungufu wa madawati
katika shule zake za msingi na kwa mujibu wa takwimu ina upungufu
wa madawati zaidi ya Milioni moja na 349.
0 comments:
Post a Comment