Meek Mill amejikuta akikiri mbele ya jaji kuwa yeye sio
Gangsta baada ya jaji kutoa kauli ya mwisho kuwa ushahidi umeonyesha wazi kuwa
amekiuka masharti yake ya kifungo chake cha nje.
Meek Mill ameongea na mahakama kwa zaidi ya saa moja akitoa
maelezo kuwa alishindwa hata kwenda kumuona mama yake alipofanyiwa upasuaji
sababu ya kukosa ruhusa ya kusafiri kutoka kwa msimamizi wa kifungi chake cha
nje.
Meek Mill pia amemuomba msamaha mwanasheria wa serikali kwa
kumwita‘Kahaba’ kwenye wimbo wake wa “The Ride.” ikiwa ni sehemu
ya kuonyesha kuwa amebadilika na sio lazima apelekwe jela tena.
Akionga na jaji Meek Mill alisema “I’m not a gangsta. I’m
not a criminal, I have my queen, Nicki [Minaj] now.I’m trying to do better and
feel like I can be the best rapper out there“.Jaji Brinkley atatoa hukumu
mwezi wa pili mwaka 2016
0 comments:
Post a Comment