Image
Image

Wafanya biashara wa nyama watoa huduma hiyo kwa mazingira magumu Tabora.


Kwa zaidi ya miaka kumi sasa wafanyabiashara katika soko la nyama mkjini Tabora wamekuwa wakitoa huduma za kitoweo hicho katika mazingira magumu kutokana na kutokuwepo na kuharibika kwa Mwandao wa maji,huku wakiingia gharama kubwa kununua maji,katika kile walichodai kuwa,manispaa ya Tabora imewatelekeza,wakati wakilipa ushuru.
Wakizungumza na mara baada ya kulipiwa zaidi ya shilingi laki nane,na mbunge wa jimbo la Tabora mjini Bw,Emmanuel Mwakasaka, kwa ajili ya kurejesha huduma  hiyo,wafanyabiashara wahao wamesema kuwa, biashara ya nyama inahitaji usafi kwa lengo la kutoa huduma safi na inayomvutia mlaji, na hivyo wamekuwa wakiingia gharama kubwa, ili kukidhi haja hiyo.
Akitoa shukrani  kwa niaba ya  wafanyabiashara hao,mwenyekiti wa soko hilo Bw.Ahamad Juma amesema kuwa, kwa ujumla soko kuu la mjini tabora limekuwa likikabioliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za uchakavu wa miundombinu na hivyo msaada huo umefika kwa wakati muafaka, huku mwakilishi wa mbunge huyo Bw,Mussa Mdaki akidai kuwa hatua inayofuata ni kurejesha umeme katikasoko hilo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment