Image
Image

Utupwaji na utelekezwaji watoto na kuishi mazingira magumu unashikasi Morogoro.



Licha ya kuwepo na upazwaji sauti na mashirika na wadau sambamba na haki za binadamu juu ya matukio ya ukatili kwa watoto ya kutelekezwa katika maeneo mbalimbali hali bado inaonekana kushika kasi kwqa Manispaa ya Mororogo ambapo hali hiyo inatajwa kuendelea na kusababisha kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wengine kupotea katika mazingira yasioeleweka.Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha mgolole manispaa ya Morogoro Sista Peragia Maria amesema idadi ya watoto wanaotelekezwa na ndugu  inaongezeka na kwamba  watoto wachanga 10 na wengine zaidi ya 50 wenye rika tofauti wanalelewa katika kituo hicho ambapo ameomba wasamariawema kujitokeza kuwasaidia mahitaji mbalimbali yatakayo wawezesha kuwatunza watoto hao.
Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Saidi mwenye umri kati ya miaka mitatu na minne akiwa ametelekezwa na wazazi wake majira ya usiku barabarani huku akieleza  wazazi wake wamemtupakufuatia changamoto zinazokikabili kituo hicho kampuni ya Mega Trade Investment Limitedi ya jijini Arusha imetoa msaada wa vyakula, mavazi, dawa za kutibu magonjwa mbalimbali kwa watoto hao pamoja na umeme wa luku vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na kwamba kampuni hiyo itaendelea kusaidia kituo hicho ili kuwapunguzia ukali wa hali ngumu ya maisha.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment