Image
Image

Rais Magufuli akutana na mwakilishi wa ADB na balozi wa Rwanda.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiteta jambo  na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 baada ya kufanya naye mazungumzo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana  na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 baada ya kufanya naye mazungumzo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene kayihura Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 na kufanya naye mazungumzo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene kayihura Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 baada ya kufanya naye mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipokutana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 na kufanya naye mazungumzo.

Katika tukio jingine rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemuhakikishia mwakilishi mkazi wa benki ya maendeleo ya Afrika AFDB Dkt.Tonia Kandiero kuwa serikali yake ya awamu ya tano itaendelea kushirikiana na benki hiyo katika utekekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
pamoja na kumhakikishia ushirikiano rais Magufuli ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unawezesha kuanza kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa huku Dkt.Tonia Kandiero akimpongeza  rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania katika awamu ya tano,amemhakikishia kuwa benki ya AFDB iko tayari Kuendelea kushirikiana na tanzania katika maendeleo kama amabavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga dola bilioni mbili nukta tatu kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pia katika hatua nyingine rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Rwanda hapa nchini Mh.Eugene Kayihura Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi kayihura amesema rais kagame amefurahishwa na hatua ambazo rais Magufuli anazichukua hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari na kumhakikishia kuwa Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa kuitumia bandari ya Dar es Salaam ambayo hupitisha asilimia zaidi ya 70 ya mizigo ya Rwanda.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment