Image
Image

Wahamiaji haramu wakutwa wametelekezwa mikumi na wanne wakiwa wamekufa.


Jeshi la polisi limewabaini wahamiaji haramu saba wanaodaiwa kutokea nchini Ethiopia wakiwa wametelekezwa kwenye gari maeneo ya Mikumi wilayani,kilosa mkoani morogoro,baadhi yao wakiwa wamepoteza maisha na wengine hali zao zikiwa ni mbaya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonarld Paulo amesema walifanikiwa kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusiana na uwepo wa wahamiaji hao haramu  eneo la mikumi,ambapo baada ya kufika walikuta wahamiaji haramu wanne wakiwa tayari wamefariki dunia huku wengine wawili hali zao zikiwa ni mbaya na mmoja akiwa mzima  ambapo baada ya kuwahoji walidai kutokea  nchini ethiopia na walikua wakielekea  Afrika Kusini kwaajili ya kujitafutia maisha.
Katika hatua nyingine polisi wanamshikilia mtu mmoja saidi mwinshee (32 ) mkazi wa kungwe tarafa ya Mkuyuni katika wilaya ya Morogoro,akituhumiwa kumkatakata kwa panga hadi kufa mamayake mzazi sikudhani mgumba mwenye umri wa miaka 70 na mkazi wa kungwe kwamadai ya kula chakula chake ampapo uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kijana huyo kuwa na matatizo ya akili.
Kwa upande mwingine jeshi la polisi mkoani hapa limetoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu nakuahidi kuwafuatilia na kuwakamata kwa hatua zaidi za kisheria,huku amanda paul akiwataka wananchi wa Morogoro kusherehekea mwaka mpya kwa amani na utulivu na ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali kukabiliana na uhalifu wowote utakaoweza kujitokeza.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment