Image
Image

Wanafunzi watakaojiunga drasa la kwanza na awali 9,943 waandikishwa Morogoro.



HALMASHAURI ya wilaya ya Morogoro na Manispaa ya Morogoro wamefanikiwa kuandikisha jumla ya wanafunzi 9,943 watakaojiunga na darasa la kwanza na shule ya awali katika kipindi cha mwaka 2016.
Wakizungumza kwenye kikao kilichohusisha maafisa elimu wa halmashauri hizo za wilaya na wadau wengine wa elimu,Kaimu Afisa elimu ya msingi katika Manispaa ya Morogoro Christopher Wangwe amesema wamefanikiwa kuandikisha wanafunzi 4,406 wakiwemo 2,978 wa elimu ya awali na 1,428 wa darasa la kwanza.
Wangwe amesema uandikishwaji huo umefanya idadi ya walioandikishwa kufikia 4,109 ni sawà na asilimia 56 ya malengo yaliyokusudiwa na kwamba asilimia 44 zilizosalia zinatarajiwa kumaliziwa katika uandikishaji unaoendelea katika kipindi cha Januari mwakani.
Naye Afisa elimu ya msingi katika wilaya ya Morogoro Donald Pambe amesema halmashauri hiyo imeandikisha wanafunzi 3,560 wa shule ya awali na 3,556 wa darasa la kwanza na kufanya jumla ya walioandikishwa kufikia 7,116.
Akizungumza katika kikao hicho,Mkuu wa wilaya ya Morogoro Muhingo Rweyemamu amewaagiza maafisa elimu na wale wote wanaohusika na elimu kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wakiwemo wale wenye umri wa hadi miaka 15 ambao wengi ni watoto wa jamii ya wafugaji wanaandikishwa shule katika elimu ya awali na elimu ya msingi.
Rweyemamu amesema wilaya hiyo ya Morogoro imezungukwa na jamii ya wafugaji na kwamba wengi wa wazazi hawana tamaduni za kupeleka watoto shule badala yake huwaelekeza kuchunga mifugo na wengine kuwakatiza masomo kwa kuhama hama,jambo ambalo Serikali haikubaliani nalo.
Amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kusomesha wanafunzi bure hivyo mzazi hana haja ya kuwa na visingizo vitakavyofanya mtoto wake kukosa elimu na kuonya watakaokaidi sheria itachukua mkondo wake kwa kuwachukulia hatua kali wazazi watakaobainika kupinga agizo hilo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment