Wananchi wa Mtaa wa Mindu,Kata ya Mindu katika
Manispaa ya Morogoeo wamewalala mikia viongozi wa eneo hilo kushindwa
kuwasomea taarifa ya mapato na matumizi,pamoja na kudaiwa kuuza maeneo
bila ya kuwashirikisha wananchi.
Baadhi ya wananchi wa mtaa huo wa Mindu wametoa malalamiko
yao wakati wa mkutano wa hadhara, uliolenga kuwajadili viongozi wao
kutoitisha vikao na kushindwa kuwasomea taarifa za mapato na matumizi yan
ayoingia katika Kata yao.
Wananchi hao pia wameon esha hofu ya kuibiwa fedha na
kutumika bila kuzingatia vipaumbele ambapo mwenyeki ti wa mtaa huo alishindwa
kutoa majibu ya kueleweka ikiwemo hoja ya ufunguaji wa akaunti .
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,MUHINGO RWEYEMAMU amewaambia
wananchi hao kuwa wao ndiyo wenye dhamana kwa kiongozi
wanayemtaka au kumkataa na wanawajibu wa kuhoji na kufahamu
taarifa za mapato na matumizi yanayokusanywa .
Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
na timu yake kuangal ia utararibu wa kufukia mashimo yanayochimbwa
mchanga katika Kata na Mtaa wa Mindu pamoja na ukusanyaji wa ushuru k wa magari
yanayobeba mchanga na kutaka kila kambi inayochimba mchanga kuwa na choo
.
0 comments:
Post a Comment