Image
Image

Waziri Kigwagala awashukia watumishi wachelewaji wiza ya Afya na kutoa msimamo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini. 
Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani. “Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla akiwambia askari wa getini. 
 Baada ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda wa kusaini kuingia umeisha. 
Baada ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe Magufuli. Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali imewaagiza kufanya. 
“Nina wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa ni kina nani huwa wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa,” alisema Dkt. Kingwangalla. 
 Aidha Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi wanakuwa hawasaini kuwa wametoka. 
 Pia alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole “Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa kufika na kuwahi kutoka ofisini.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa kila idara za wizara hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku zilizopita.
 Mmoja wa wasaidi wa idara ya rasilimali watu akimkabidhi vitabu vya mahudhurio Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
 Askari wa getini wakimpa maelezo mmoja wa watumishi wa wizara hiyo kuwa Mh. Naibu Waziri ameagiza watumishi wote waliochelewa kuzuiliwa kuingia ndani.
Magari ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya kutambua kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Kigwangalla ametoa agizo la kuizuia watumishi wachelewaji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment