Rafiki wa wapenzi waliotekeleza mashambulizi na
kusababisha mauaji ya watu 14 mjini San Bernardino huko California nchini
Marekani mwanzoni mwa mwezi huu amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya
kushirikiana kufanya kosa la ugaidi.
Enriquez Marquez anashutumiwa kununua silaha mbili
kinyume cha sheria ambazo zilitumika na Syed Rizwan Farok na Mkewe Tashfeen
Malik pia alinunua malighafi iliyotumika kutengeneza Bomu.
Marquez amekana mashtaka akisema kuwa hakufahamu
mipango ya wapenzi hao.
Mtu mwingine Jalil bin Ameer Aziz amekamatwa
pennyslvania kwa kosa la kushiriki na kujaribu kutoa msaada wa mali kwa kundi
la Islamic state
wapelelezi wanasema Enriquez alibadili dini na kuwa
muislamu baada ya kufahamiana na jirani yake Syed Rizwan Farook.
Inaelezwa kuwa walikuwa wakitazama picha za video
zinazohusiana na maswala ya itikadi kali za kiislamu na walipanga mipango ya
mashambulizi ya kigaidi mwaka 2011 na 2012 huko califonia.
Maafisa upelelezi wanasema kuwa wapenzi walipanga
kurusha mabomu katika mgahawa wa wanafunzi kabla ya kufanya mashambulizi kwa
risasi . Pia walipanga mipango ya kushambulia abiria wakiwa kwenye magari
wakati wa muda wa pilika nyingi.
Enriquez mwenye umri wa miaka 24 anatuhumiwa pia kwa
udanganyifu kuingia kwenye ndoa ya udanganyifu na mmoja wa mwanafamilia wa
Farook.kwa makosa matatu yanayomkabili iwapo atakutwa na hatia atahukumiwa
kifungo cha jumla ya miaka 35 gerezani.
0 comments:
Post a Comment