afya ni uhai na
kadri utakapo jali afya yako basi unaongeza siku zako za kuishi vizuri
zaidi hapa duniani.
Lishe bora ni muhimu sana kuzingatiwa na ni vyema kufuata taratibu
na miiko ya lishe na kwa kawaida baada ya mlo tumbo linakuwa limejaa mtu
anajisikia kulala au kafanya jambo lolote jingine .
Kufuatia hali hiyo kuna baadhi ya vitu havishauriwi kufanywa baada ya
mlo na vinapofanyika huweza kuwa sababu ya kuharibu afya zetu.
Moja ya mambo ambayo hayapaswi kufanyika mara baada ya kula ni pamoja
na kulala baada ya mlo mwanadamu kwa kawaida binadamu anapaswa kulala
masaa 3 baada ya mlo wake ,iwapo akalala kabla ya hayo masaa sio vizuri
kiafya, kwani chakula kinatakiwa bado hakijasagika vizuri tumboni jambo
ambalo huweza kupelekea kuongezeka kwa uzito kwa haraka.
Kuoga baada ya mlo pia si vizuri kwani huchangia kusababisha
kucheleweshwa usagaji wa chakula mwilini ,damu sehemu ya tumboni
inakuwa inasafirishwa sehemu nyingine za mwili haswa mguuni na mikononi
pindi uogapo badala ya damu kutumika kwenye mmeng’enyo wa chakula,
hivyo ni vyema ukaoga kabla ya kula.
Pia kuvuta sigara baada ya mlo huchangia kuharibu mfumo wa 'digestion' kwa urahisi kupitia sumu ya sigara.
Kunywa chai baada ya mlo sio vizuri , kwani humfanya mhusika kupoteza
baadhi ya madini na kunyonywa kwa urahisi kama madini ya chuma n.k ni
vyema ukanywe chai mara baada ya saa1 baada au kabla ya mlo ndio sahihi
kwa afya yako.
Kufanya mzoezi baada ya mlo ni makosa subiri
ipite saa 1 au 2 ndio ufanye mazoezi hali hiyo huweza kuchangia utumbo
kushindwa kusaga chakula vizuri.
Kukaza mganda za suruali baada ya mlo
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment