Image
Image

Bodi ya kudhibiti video na filamu nchini Kenya (KFCB) imepinga hatua ya kampuni ya Netflix.

Bodi ya kudhibiti video na filamu nchini Kenya (KFCB) imepinga hatua ya kampuni ya Netflix kuanza kutoa huduma zake nchini Kenya.
Bodi hiyo imesema Netflix, kampuni inayouza video na filamu kupitia mtandao, ni lazima ipate kibali cha kuhudumu nchini Kenya kabla ya kuanza kutoa huduma.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Askofu Jackson Kosgei amesema video za Netflix hazijachunguzwa na kuorodheshwa kwa mujibu wa viwango vya filamu vya Kenya.
Amesema katika baadhi ya video walizotazama, ingawa hakuzitaja, zilikuwa zimeorodheshwa kwamba zinafaa kwa watoto wa umri wa miaka 13 lakini baada yao kuzitazama wakabaini zina picha za uchi, zinatumia lugha chafu na zinatukuza matumizi ya dawa za kulevya.
“Tuna wajibu wa kuwalinda watoto na vijana wasionyeshwe picha na video zinazoonyesha matukio ya vurugu na ukatili na zinazochochea uchi na kushiriki ngono,” amesema Askofu Kosgei.
Bodi hiyo pia imesema katika mazingira ya sasa ambapo ugaidi umekuwa tatizo kuu, serikali ina haki ya kufuatilia video ambazo watoto na vijana wanatazama wasije kukumbatia itikadi kali.
Hatua ya bodi hiyo inaonekana kuenda kinyume na ushauri wa waziri wa habari na mawasiliano Bw Joe Mucheru ambaye wiki iliyopita alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akishauri idara za serikali kusubiri mwongozo kutoka kwa serikali.
Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya nayo pia ilikuwa imesema Netflix haiwezi kudhibitiwa chini ya sheria za utangazaji Kenya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment