Image
Image

Juice ya miwa inauwezo mkubwa sana wa kupambana na saratani.



Kuna baadhi ya vinywaji huwa tunakutana navyo katika mazingira ya maisha yetu ya kawaida kabisa, na hata gharama zake ni kawaida pia, lakini uzuri wake na thamani yake kwa afya ni zaidia ya mazingira na gharama ya upatikanaji wake.
Hapa nataka kuzungumzia juisi ya miwa ambayo ukikatiza baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam basi utakutana nayo sana na imekuwa na wapenzi wengi licha ya kwamba wengu hunywa kama kiburudisho tu wasijue kuwa juisi hiyo huwa na manufaa kwa afya zao.
Mtaalam wa tiba asili jijini Dar es Salaam, Tabibu Abdallah Mandai, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa miwa ina faida nyingi katika afya likiwamo hili la uwezo wake mkubwa wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya 'glucose' inayopatikana ndani yake.
Mtaalam huyo, anafafanua kuwa, kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kiasi cha 'kalori' 11 madini halisi pamoja na vitamin ambazo zinapatikana ni kama 'phosphorus', 'calcium,' madini ya chuma na 'potassium.'
Hata hivyo, Tabibu Mandai anasema miwa inauwezo mkubwa sana wa kupambana na saratani hususani ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya matiti, uwezo wake huo unaotokana na kuwa miwa ni jamii ya tunda lenye alkali.
Mbali na hayo, virutubisho vilivyopo katika miwa huwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu mwilini kama moyo, ubongo, figo na viungo vya uzazi.
Hali kadhalika miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini na inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment