Image
Image

Julio amesema timu yake ilicheza kwa kiwango kibovu kilichosababisha kupoteza mchezo wake.

KOCHA wa Mwadui, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ amesema timu yake ilicheza kwa kiwango kibovu kilichosababisha kupoteza mchezo wake dhidi ya Mbeya City.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya juzi, Mwadui Fc ilikubali kichapo cha bao 1-0.
Akizungumza na gazeti hili, Kihwelu alisema Mbeya City ilistahili kupata ushindi huo kwa kuwa ilicheza vizuri kuliko timu yake.
“Mpira una matokeo matatu, kufunga, kupata sare na kufungwa, tumefungwa na Mbeya City na nasema walistahili kushinda kwa sababu walicheza vizuri na kupata nafasi moja iliyowapa ushindi,” alisema.
Kihwelu alisema kupoteza mchezo huo hakuwakatishi tamaa katika mbio zao za kupambania taji la ubingwa kwani bado kuna michezo mingi mbele na kwamba wakijipanga watafanya vizuri.
Mwadui Fc kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 nyuma ya Prisons wenye pointi 24.
Timu hiyo imecheza michezo 14, ikishinda michezo sita, ikipata sare nne na kupoteza minne.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment