Image
Image

Wakazi zaidi ya 400 hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba 70 kusombwa na mafuriko Dodoma.

Wakazi zaidi ya 400 hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba 70 kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la kijiji cha Mpunguzi kilichopo Manispaa ya Dodoma.
Baadhi ya wakazi waliokumbwa na mafuriko hayo wamesema hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa kile wanachodai ni udogo wa daraja lililopo barabara kuu ya Dodoma Iringa linalokatisha eneo hilo kushindwa kuhimili wingi wa maji na kujenga mkondo ambao umesambaa na kuyafikia makazi yao na kuzua balaa hilo ..
Kufuatia janga hilo kaimu afisa mtendaji wa kijiji cha Mpunguzi Dionuis Samo amesema mafuriko hayo ambayo ni mara ya pili kutokea kwa kipindi cha wiki mbili ameiomba serikali kupitia wakala wa barabara nchini TANROADS kulitafutia ufumbuzi wa haraka eneo hilo ili lisiendelee kuleta madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma…
Mvua hizo pia zimeripotiwa kusababisha maafa katika kata za Kigwe wilayani Bahi, Nzuguni Manispaa ya Dodoma na kijiji cha Matumbulu ambapo kwa mujibu wa viongozi wa serikali katika maeneo hayo wanadai zaidi ya watu 400 wameathirika .

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment