Image
Image

Shukrani kwa wasomaji wa Taarifa zetu na Pongezi kwa Rais Dkt.Magufuli.



Uongozi mzima wa Tambarare Halisi unawatakieni Hery ya Mwaka mpya 2016,na kutoa shukrani za dhati kwa kutuamini na kuwa wenye kusoma taarifa zetu kila zinapo tufikia hivyo mmezidi kutupa moyo wa kuendelea kuwapasha habari kila muda zitufikiapo.
Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka ambao kila mmoja aliuona ni mwepesi na wengine kuona mgumu kwa kutofikisha lengo,nivyema sasa kwa mwaka 2016 kujipanga upya ilikuweza kukamilisha lengo.
Vilevile tunapenda kumpongeza Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa na kuanza kasi aliyoiahidi ya hapa kazi tu kwa kutumbua majipu ndani ya serikali na taasisi mbalimbali kwa ukwepaji kodi na matumizi makubwa ya fedha yanayoligharimu taifa na kuboresha sekta za afya na huduma za afya  kuanza kupatikana mara moja
Tunapenda kuona kwamba kwa kasi ya Rais Magufuli kwa mwaka 2016 inapewa nguvu kuanzia watendaji ndani ya serikali na jamii kiujumla ili tupate Tanzania mpya na yenye muonekano mpya kwa wananchi kuanzia hali ya chini.
Pia mgogoro wa kisiasa Zanzibar ambao haujapata muafaka toka mwaka jana licha ya vikao vingi kufanyika vya ndani ya serikali ya Zanzibari hadi hivi leo ni faraja yetu tukija kuona kwa mwaka huu Kasi hii ya hapa kazi tu itatue maramoja kusudi tuwe wa moja na tujenge nchi kwa pamoja.
Mwaka jana 2015 Mwezi wa kumi na mbili licha ya kuwa viongozi wote wa serikali ya Zanzibar wanao vutana kwa kila mmoja alionana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nakumueleza kila hatua inavyoendelea kwenye vikao vyao vya ndani ili kukubaliana na kumaliza mgogoro huo lakini bado nadhani haitoshi kwa mwaka huu ni vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ukaona ninamna gani hili suala linamalizika na kubaki historia kwani naamini hakuna kinachoshindikana pakiwa na mazungumzo yenye mrengo wa amani na tija ya kujenaga taifa.
Kila la Kheri Tumpe Nguvu Rais afanye anayoyakusudia nasi tunaahidi tutakuwa naye bega kwa bega.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment