Image
Image

Simba na Azam kuoneshana ubabe leo.

TIMU za Simba na Azam leo zinashuka katika viwanja tofauti katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Simba itakuwa mgeni wa JKT mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wakati Azam FC itakuwa mgeni wa Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 30, Azam ya pili ikiwa na pointi 36 sawa na vinara Yanga wakitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mchezo wa Dar es Salaam unazikutanisha timu mbili zenye mazingira tofauti, ambapo imetoka kushinda mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar bao 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa chini ya Kocha Msaidizi Jakson Mayanja.
Hata hivyo inakutana na JKT Ruvu, ambayo imetoka kupata kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga, ambacho kiliwastua kwa kuwa walikuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kutokana na hali hiyo ni wazi Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni atataka kushinda ili kuiweka sawa timu yake.
Kwa upande wa Azam inayokutana na Mgambo itakuwa na kibarua kizito kutokana na timu hiyo kuwatesa vigogo kwenye uwanja wao wa Mkwakwani. Timu hizo ziliwahi kukutana wakati Azam ikijiandaa na maandalizi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi ambapo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mkoani huko.
Pia, Azam imetoka kupata sare dhidi ya African Sports ya Tanga katika mchezo wa ligi uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Kama Azam itateleza leo kisha Yanga ikashinda kesho dhidi ya Majimaji itakuwa imeweka pengo kubwa kati yake na Yanga.
Mechi nyingine leo itakuwa kati ya Ndanda FC ikiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Ndanda sio timu rahisi licha ya kuwa hawako katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi, wamekuwa wakitingisha timu kubwa. Pia, Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Timu hiyo ya Tanga iko kwenye hatari ya kushuka daraja, hivyo ushindi ni muhimu kuhakikisha inajinasua kwenye hatari. Kwa upande wa Stand United itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Timu hizi zinajuana na zimekuwa zikionesha kandanda safi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment