Image
Image

DILI la wachezaji wa Azam FC ngoma nzito.

DILI la wachezaji wa Azam FC, Kelvin Friday na Farid Mussa kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania limekuwa gumu.
Friday alifuzu kucheza katika klabu ya St. George ya Ethiopia baada ya kwenda kufanya majaribio ya wiki mbili hivi karibuni, wakati Mussa alikuwa anatakiwa na timu moja ya Slovenia iliyokuwa imeweka kambi Hispania.
Akizungumza na gazeti hili, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema kuwa Friday baada ya kufuzu, timu hiyo ya Ethiopia ilisema ingekuja kufanya mazungumzo lakini haifanya hivyo.
“St. George ilionesha nia kwa sababu mchezaji alishafuzu, lakini baadaye hawakuonekana tena, kwa hiyo mchezaji mwenyewe kwa sababu tulimpeleka Mtibwa kwa mkopo tukamwambia aendelee na timu hiyo,” alisema.
Aidha, kwa upande wa Mussa, Kawemba alisema wakati timu iko Zanzibar walikuwa wakimhangaikia mchezaji na alikuwa tayari amepata hati ya kusafiri, lakini kilichotokea kuna baadhi ya vitu walitakiwa kuwa navyo.
“Mambo yalikuwa yanaenda vizuri, tulipata hati ya safari kule ubalozini lakini kuna vitu walihitaji tuwape na kwa wakati huo hatukuwa navyo, kwa hiyo nikamwambia mchezaji aende Zanzibar kujiunga na wenzake na baadaye tutaendelea,” alisema.
Kawemba alisema kwa vile Mussa bado umri wake ni mdogo wataendelea kumuimarisha kiwango chake kwa kuwa bado kuna timu za Ulaya zimeonesha nia ya kumhitaji na mambo yakiwa sawa wataweka wazi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment