Image
Image

Tanzania ipo tayari kushirikiana na Israel katika nyanja za kiuchumi.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemhakikishia Waziri Mkuu wa Israel kuwa Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kushirikiana na kuimarisha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na Israel katika nyanja mbalimbali ili kuleta manufaa kwa pande zote.
Rais Magufuli amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi - Kenya Mheshimiwa Yahel Vilan, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Aidha Rais Magufuli ameahidi kuwa Tanzania itahakikisha inaanzisha ubalozi wake nchini Israel haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake Balozi wa Israel hapa nchini Yahel Vilan pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanywa na uongozi wake katika kipindi kifupi cha miezi miwili tangu aingie madarakani amemuhakikishia kuwa Israel itaendelea kushirikiana na Tanzania na ipo tayari kuimarisha zaidi mahusiano yake.
Balozi Vilan ametaja baadhi ya maeneo ya ushirikiano kuwa ni pamoja Kilimo,Maji,Ufugaji wa Nyuki na Sayansi na Teknolojia huku akibainisha kuwa Israel imewaalika jumuia ya wafanya biashara wa Tanzania kushiriki katika kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Israel litakalo fanyika mjini Tel Aviv nchini Israel Mwezi Septemba Mwaka huu.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Yahel Vilan wa Israel hapa nchini  Ikulu Jijini Dar es salaam Januari 19, 2016 baada ya kufanya naye  mazungumzo
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Balozi Yahel Vilan wa Israel hapa nchini kabla ya kufanya naye  mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Januari 19, 2016
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment