Image
Image

Abiria 100 watekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan


Wanamgambo wa kundi la Taliban wameripotiwa kuteka nyara mabasi mawili yaliyokuwa yamebeba abiria 100 waliokuwa wakisafiri kuelekea Kabul kutoka mkoa wa Faryab nchini Afghanistan.
Mkuu wa polisi mkoani Faryab Sayid Aaka Anderabi, alitoa maelezo na kuarifu kwamba wanamgambo hao waliyasimamisha mabasi hayo ya abiria katika mji wa Karamkol ulioko mkoani Mirzakum.
Mahali walikopelekwa abiria hao waliotekwa nyara bado hakujajulikana.
Anderabi aliongezea kusema kwamba maafisa wa usalama wameanzisha shughuli zao kwa ajili ya kuwaokoa abiria hao waliotekwa nyara.
Kundi la Taliban halijatoa maelezo yoyote kuhusiana na tukio hilo.
Takriban miezi 6 iliyopita, kundi la Taliban pia liliwahi kuteka nyara basi moja lililokuwa na abiria 12 katika mji wa Gazne nchini Afghanistan.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment