Image
Image

Kenyatta ametoa shutuma kali dhidi ya raia wake kuhusu jinamizi la ufisadi Kenya.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa shutuma kali dhidi ya raia wake kuhusu jinamizi la ufisadi akiwa kwenye ziara rasmi ng'ambo.
Akihutububia kundi la Wakenya wanaoishi nchini Israel, Rais Kenyatta alisema ni jambo la kusikitisha kwamba taifa la Kenya linasifika kwa mambo mabaya ikiwa pamoja na ufisadi uliokithiri, ukabila wa hali ya juu na matusi yanayoendelezwa hasa na wanasiasa.
Rais Kenyatta yumo katika ziara rasmi nchini humo.
“Sisi kama Wakenya pia, Mungu ametupatia nchi ambayo ni nzuri mara 20 kuliko hii tuko hapa (Israel). Lakini tukitembea ni kulia, ni kuiba ...,” alisema.
“… tuko na ujuzi pia, ya kuiba, ya kutukanana, ya kufanya mambo mengine maovu, ya kuleta ukabila.
Bw Kenyatta alisema licha ya Kenya kuwa taifa lenye utajiri mkubwa, kasumba ya ufisadi miongoni mwa viongozi na raia imelemaza ustawi wa taifa hilo.
Kukiri kwa Rais Kenyatta akiwa ziarani Israel kwamba ufisadi umemea mizizi katika taifa lenye uchumi bora zaidi kanda ya Afrika Mashariki, kunajiri huku jinamizi hilo likiendelea kugonga vichwa vya habari, na kutawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya.
Kashfa ya mamilioni ya pesa kuporwa kutoka mfuko wa huduma ya vijana wa taifa (NYS) na vigogo serikalini, ndiyo sakata ya ufisadi ya hivi karibuni inayokumba utawala wa Rais Kenyatta.
Mwaka jana, Kenyatta aliwapiga kalamu mawaziri watano na maafisa wengine wakuu serikalini kutokana na madai ya ulaji rushwa.
Majuzi Jaji Mkuu Dkt Willy Mutunga alizua mjadala mkali mitandao ya kijamii baada yake kunukuliwa na gazeti la Uholanzi akisema kwamba Kenya ni taifa la “wanyang’anyi”.
Dkt Mutunga alinukuliwa akisema kwamba wananchi wanapigana vita na magenge ya watu sawa na ‘mafia’ ambayo yanaongozwa na viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wafisadi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment