Image
Image

Ugiriki yatishia kupinga maamuzi ya viongozi wa umoja wa ulaya kuhusu wahamiaji.

Ugiriki imetishia kupinga maamuzi yote katika mkutano ujao wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu uhamiaji iwapo nchi wanachama hazitakubaliana kugawana kwa uwiano wahamiaji na wakimbizi.
Hatua hiyo imekuja wakati Austria na baadhi nchi za Balkani kutoa wito kupunguzwa kwa wahamiaji wanaovuka mipaka ya nchi zao.
Akihutubia bunge mjini Athens Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema haikubaliki kwamba nchi yake iachiwe kukabiliana na tattizo hilo pekee yake.
"tunachokataa kufanya ni kukubali mabadiliko katika nchi yetu kuwa ghala kubwa la nafsi za watu , na wakati huo huo tuendelee kuchukua hatua ndani ya Umoja wa Ulaya na katika mikutano ya viongozi wa Umoja huo kana kwamba hakuna jambo lolote baya. Kuanzia sasa na kuendelea Ugiriki haitakubalina na makubaliano kama hatutahakikishiwa mgawanyo wa uwiano wa mzigo na wajibu wa makazi ya wakimbizi miongoni wa nchi wanachama."
Wakati huo huo mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya zinakutana mjini Brussels asubuhi hii kuzunguzia suala la tatizo la wakimbizi huku onyo likitolewa kama tatizo hilo litaendelea itakuwa vigumu kulishughulikia.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kufanya mikutano miwili kuhusu suala la wahamiaji mwezi ujao ili kujaribu kuwa na sera kabla wimbi jingine la wahamiaji.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment