Image
Image

Mameneja wa Tanesco wanaosuasua katika uwajibikaji kutimuliwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa Mameneja wa Shirika la umeme nchini TANESCO wanaosimamia Kanda mbalimbali nchini wataondolewa katika vyeo hivyo iwapo hawatatimiza maagizo mbalimbali waliyopangiwa na Wizara ya Nishati na Madini ifikapo machi moja mwaka huu.
Profesa Muhongo amesema hayo wakati wa kikao chake na watendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.
Katika kikao hicho Prof. Muhongo amesema atawaondoa katika nafasi zao Mameneja wa Tanesco watakaoshindwa kuunganisha huduma kwa wateja wengi, kuwa na makusanyo makubwa ya bili za umeme, kupunguza manung’uniko ya wananchi katika huduma za umeme na uboreshaji wa mawasiliano kati ya Shirika hilo na wananchi
Mbali na hilo amewataka mameneja hao kutumia vyombo vya habari kuelemisha wananchi juu ya masuala ya umeme.
Aidha, Waziri wa Nishati na Madini amekitaka Kitengo cha Uwekezaji cha Tanesco kama hakitakuwa na miradi mipya ya umeme ifikapo tarehe 2 Aprili mwaka huu, watendaji katika Ofisi hiyo wataondolewa katika nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Vilevile Profesa Muhongo amewaagiza watendaji wa TANESCO katika vitengo vya ukaguzi kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo usimamizi madhubuti wa nguzo za umeme ambazo baadhi huanguka kila inapofika msimu wa mvua na kusema kuwa suala hilo halikubaliki.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment