Image
Image

Marekani na Russia zatangaza mpango wa kukomesha mivutano yao nchini Syria.

Marekani na Russia zimetangaza mpango wa kukomesha mivutano yao nchini Syria kuanza jumamosi, kwenye makubaliano ambayo Umoja wa mataifa umeyataja kuwa ni "dalili ya matumaini" ya kukomesha mgogoro wa miaka mitano nchi Syria. Hata hivyo makubaliano hayo, ambayo hayahusishi makundi ya IS, Al Nusra na makundi mengine yaliyoorodheshwa na umoja wa mataifa kuwa ni makundi ya kigaidi, bado yanasubiri kuidhinishwa na serikali ya Syria na makundi ya waasi.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Marekani na Russia inasema, kundi lolote linalohusika kwenye mgogoro wa Syria litaiarifu Marekani au Russia utayari wao wa kusimamisha mapambano kabla ya jumamosi. Makubaliano hayo kuhusu usimamishwaji wa mapambano, ulihimizwa na mkutano wa Munich wa kundi la uungaji mkono wa Syria ISSG linaloundwa na nchi za umoja wa kiarabu, Umoja wa Ulaya, Umoja wa mataifa na nchi nyingine 17 ikiwa ni pamoja na China.
Hata hivyo makubaliano hayo yalishindwa kuanza kutekelezwa kwa muda uliopangwa, kutokana na tofauti kati ya Marekani na Russia zinazoziunga mkono pande zinazopambana nchini Syria. Utatanishi zaidi umetokea kutokana na ugumu kwa Marekani kuzishawishi washirika wake wakubwa wa mashariki ya kati Uturuki na Saudi Arabia, kushiriki kwenye mazungumzo. Saudi Arabia imekuwa ikitishia kuwa itatuma vikosi vyake kupambana na jeshi la Syria, wakati Uturuki imeshaanza kuwashambulia wakurd wanaopambana na wapiganaji wa kundi la IS.
Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Ban Ki Moon amekaribisha makubaliano hayo, na kuyataja kuwa ni ishara ya matumaini kwa watu wa Syria, kwamba uchungu walioupata kutokana na vita ya miaka mitano sasa unakaribia kwisha. Rais Vladmir Putin wa Russia amesema makubaliano hayo ni hatua halisi kuelekea kukomesha vita, na Rais Barack Obama wa Marekani amesema kwa sasa kipaumbele ni kwa serikali ya Syria na makundi ya upinzani kutekeleza makubaliano.
Habari iliyotolewa na vyombo vya habari vya Syria inasema makubaliano hayo kati ya Marekani na Russia yamekubaliwa na Serikali ya Syria.
Habari hiyo imenukuu taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ikisema, jeshi la serikali litasimamisha operesheni za kijeshi, lakini litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi IS na Al Qaede.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment