Image
Image

UN yazitaka pande zote za Syria kuanza mazungumzo ya amani.


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likilaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mjini Damascus na Homs, Syria na kusema uwepo wa kundi la IS umeathiri vibaya utulivu na hali ya haki za binadamu nchini Syria. Baraza hilo pia limetoa wito kwa pande zote kuanza tena mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo.
Habari kutoka Ikulu ya Ufaransa zinasema viongozi wa Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Uingereza jana walijadiliana kwa njia ya simu kuhusu makubaliano ya kusimamisha vita nchini Syria yaliyofikiwa kati ya Marekani na Russia na kutarajia kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa haraka.
Wakati huohuo, waziri wa maridhiano ya kitaifa wa Syria Bw Ali Haidar amesema, serikali ya Syria imekubali makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Russia, lakini makubaliano hayo hayataathiri mapambano ya Syria dhidi ya ugaidi


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment