Image
Image

Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC cha Uganda akamatwa tena.

Polisi nchini Uganda wamemkamata tena aliyekuwa mgombea urais na kiongozi wa chama cha upinzani cha FDC cha Uganda Bw. Kizza Besigye ili kuepusha machafuko baada ya uchaguzi mkuu.
Bw. Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi wa rais, na kutoa wito wa kufanya maandamano ya amani. Amesema uchaguzi huo haukuwa wa haki na wazi, na unapaswa kuangaliwa na tume maalum ya kimataifa.
Habari zinasema, baadhi ya nchi za magharibi zinadai kuwa uchaguzi huo uliofanyika alhamis iliyopita ulitawaliwa na rushwa na matumizi mabaya ya polisi. Lakini rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha madai hayo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment