Image
Image

Mawaziri waanza kurudisha fomu,wengine washangaa majina yao kutajwa.


Baada ya muda mchache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli kutoa Agizo kwa  mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo saa 12.00 jioni hatimaye limeanza kutekelezwa.
Kutekelezwa huko kumekuja Baada ya waziri mkuu kutaja majina ya mawaziri wanne na naibu waziri mmoja ambao hawajarudhisha fomu za Sekretariati ya maadili ya umma na kutakiwa wawe wamerejesha fomu hizo  leo
Baada ya agizo hilo sasa aliyerudisha fomu hizo ni waziri wa mambo ya nje,ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe.Balozi Dkt.Augustine Mahiga ambapo amekiri kuwa ni kweli alikuwa hajarudisha fomu hizo kutokana na majukumu ya kazi yaliyokuwa yamembana
Baada ya zoezi hilo kutolewa muda wa kurudisha na Rais Magufuli waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga ambaye naye ametajwa kutorudisha fomu hizo ameonekana kushangazwa na jina lake likitajwa wakati ameshazirudisha na kwa sasa  ameelekea ofisi za Sektretariati ya maadili kuwasilisha malalamiko yake.
Katika hatua nyingine naibu waziri wa ofisi ya makamu wa rais,Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina amesema kuwa atawahisha kurudisha fomu hizo kabla ya saa kumi na mbili jioni.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment