Image
Image

Mchezaji wa Trabzonspor amwonesha refa kadi nyekundu Uturuki

Mchezaji wa klabu ya Trabzonspor, Salih Dursun, alitolewa nje kwa kumuonyesha mwamuzi kadi nyekundu wakati wa mchezo waliofungwa mabao 2-1 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 86 ya mchezo, klabu hizo zikiwa zimetoshana nguvu 1-1, baada ya mwamuzi Denis Bitnel kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Luis Cavanda kwa kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari. Aidha, aliwazawadi Galatasaray penalti.
Trabzonspor walikuwa tayari wamesalia wachezaji tisa uwanjani kabla ya kutokea kwa kisa hicho.
Wachezaji wa Trabzospor walimzingira mwamuzi kupinga kadi hiyo.
Ni wakati huo ambapo Dursun alimnyang’anya refa kadi nyekundu aliyokuwa nayo na kumuonyesha kadi hiyo hatua ambayo ilipelekea na yeye kufukuzwa uwanjani.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuingia katika mizozo na waamuzi, kwani Novemba mwaka jana mwenyekiti wao Ibrahim Haciosmanoglu alifungiwa siku 280 baada ya kuwafungia waamuzi wanne uwanjani kwa kushindwa kutoa penati kwa timu hiyo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment