Image
Image

Mourinho:Sijui kwa ntakuwa mkufunzi wa kilabu ya Manchester United.

Aliyekuwa mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa hajui iwapo atakuwa mkufunzi wa kilabu ya Manchester United lakini anatumai kwamba atapata ajira ya kuifunza kilabu nyengine mwishoni mwa msimu huu.
Mapema mwezi huu BBC iliripoti kwamba Mourinho amekutana na maafisa wa kilabu ya Manchester United.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53 alifutwa kazi mnamo mwezi Disemba,miezi saba baada ya kushinda kombe la ligi kuu nchini Uingereza.
Na alipoulizwa iwapo atachukua mahala pake Luis Van Gaal katika uwanja wa Old Trafford,Mourinho alijibu: ''hilo ni swali kubwa sana''.
Akizungumza katika shule moja nchini Singapore,aliongeza:Hakuna mtu anayejua na mimi ni wa kwanza kutojua,nasoma kuhusu mambo mengi tofauti.Ninaangalia siku za usoni na shauku nyingi.Kwa sasa nafurahia maisha yangu ya faragha wakati huu ambao siko kazini na natumai kwamba nitarudi mwishoni mwa msimu huu.Iwapo nataka kurudi kesho nitarudi kesho.Nadhani ni muhimu kusubiri badala ya kukimbiliajambo.
Nitaanza msimu ujao na kilabu mpya na mradi huo nadhani ni mzuri sana kwangu mimi.
Manchester United ni ya tano katika ligi ya Uingereza,ikiwa iko alama sita nyuma ya Kilabu ya Manchester City ambayo iko katika nafasi ya tano.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment