Image
Image

Mwalimu aliyefukuzwa kazi kwa kumpa mimba mwanafunzi aishi darasani kwa miaka 10.

Mwalimu wa shule ya msingi Mwagimaji iliyopo kata ya Nyanguku Mjini Geita Hamis Mumwi anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi kisha kumuoa ameendelea kuishi katika darasa moja lililopo katika shule hiyo na familia yake takribani miaka 10 licha ya kufukuzwa kwa kosa hilo.
Mwalimu huyo imedaiwa alifukuzwa mwaka 2002 na amekuwa akiishi katika darasa hali ambayo imechangia wanafunzi wa shule hiyo kuwa na vyumba vichache na kusababisha darasa moja kukaa wanafunzi wa madarasa tofauti.
Shule ya Mwagimagi ina jumla ya wanafunzi 418 na madarasa sita lakini kwa sasa yamebaki matano kutokana na mwalimu kuishi darasani.
Mwalimu Mumwi anaishi hapo baada ya nyumba alokuwa anaishi kubomoka na kuhamia darasani na hatoki hadi hapo Halmashauri itakapomlipa stahiki zake.
 Mumwi amekataa kuwa hakuoa mwanafunzi bali alimaliza darasa la saba na hakuendelea na masomo ndipo alimpa mimba na kumuona.
Amedai alifukuzwa kazi mwaka 2002 baada ya kushindwa kesi kwenye mahakama ya mwanzo lakini baadae alikata rufaa na kushinda kesi kwenye mahakama ya wilaya na mwajiri kutakiwa kumrudisha kazini ambapo alirudi hadi mwaka 2005 alipofukuzwa tena kwa mara ya pili.
Diwani wa Kata ya Nyanguku Elias Ngole aliliibua suala hili katika kikao cha Baraza la Madiwani mbapo Mwenyekiti wa Halmashauri alitaka hatua zaidi zichukuliwe.
Diwani Kata ya Nyanguku Elia Ngole amesema Imeonekana kuwa mwalimu Mumwi alipofukuzwa taratibu zote za kisheria zilifanyika ikiwemo kumsafirisha na familia yake kwenda kwao ukerewe lakini alirudi shuleni hapo.
Afisa utumishi wa halmashauri ya mji Laurence Mhelela amebainisha kuwa Mumwi hadai stahiki zozote kwa kuwa alifukuzwa kazi toka mwaka 2005 lakini kwa sasa wanachukua hatua za kulimaliza suala hilo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment